HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

May 08, 2026

WANANCHI KAGERA WATAKIWA KUZINGATIA KANUNI ZA AFYA

NA EDITHA  WILLIAM BUKOBA, KAGERA


Wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera wameshauriwa kuzingatia kanuni za afya ili kuepuka magonjwa ya mlipuko hasa katika kipindi hiki ambacho mvua zinaendelea kunyesha.


Hayo yamezungumzwa na Mganga Mkuu wa halmashauri ya Manispaa ya bukoba Mkoani kagera Dkt Peter Mkenda wakati akiwa ofisini kwake ambapo amesema kuwa wananchi wahakikishe maji yanayotumika yanakuwa safi na salama ikiwa ni sambamba na maji hayo kuchemshwa ili kuua wadudu wanaoweza kuhatarisha afya.


" niendelee kuwasihi wananchi kuwa maji yanayotumika wahakikishe yanakuwa safi na salama yanayotoka bombani, wakilazimika kutumia maji ya chemchem, mto au ziwani  basi yachemshwe au watumie vidonge vya kutibia maji".


Aidha Dkt Mkenda amesisitiza kuwa mboga na matunda yanayotoka shambani yaoshwe vizuri ili kuondoa uchafu na wadudu kabla ya kutumika ili yasilete madhara kwa mtumiaji ikiwa ni sambamba na kufunika vyakula wakati wote ili kuepuka inzi wasichafue 

"Hii hali ya hewa inasaidia kuzaliana kwa wadudu waenezao magonjwa mfano nzi wanazliana kwa wingi kipindi hiki cha unyevunyevu, na wadudu hao wamekuwa sehemu ya kusafirisha vimelea vya magonjwa kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kwahiyo vyakula visipofunikwa vizuri kuna athari ya kupata maambukizi".


Vilevile amesema kuwa jamii ikumbuke kunawa mikono mara kwa mara kabla ya kula na baada ya kutoka chooni kwa maji tiririka na sabuni kwani hii itasaidia kuondoa vimelea na vijidudu vinavyokuwa kwenye mikono

No comments:

Post a Comment

Pages