HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 30, 2013

SUMA LEE: SIJUI NIANZE NA NGOMA GANI


Na Elizabeth John
BAADA ya kutamba na wimbo wake wa ‘Apate Raha’, msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ismail Sadick ‘Suma Lee’, anajipanga kuachia wimbo wake mmoja kati ya nyimbo tano ambazo ameziandaa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Suma Lee alisema katika stoo yake ana nyimbo zaidi ya nne, ambazo ameziandaa na hajui aanze kuitoa ipi kutokana na ubora zilizonazo.

Alisema baadhi ya nyimbo ambazo tayari amezirekodi ni ‘UK Dubai’, ‘Moyo Safi’, ‘Nimekaa’, ‘Hesabu za Mapenzi’ na ‘Ndoa’, hivyo bado yupo kwenye wakati mgumu, aanze na upi.

“Baadhi ya mashabiki wanasema nimeishiwa mistari, wengine wanasema sitaki ‘Hakunaga’ ichuje ndiyo maana sitoi wimbo mwingine, naomba mkae mkao wa kula, vitu vizuri vinakuja,” alisema Suma Lee.

Mbali na vibao hivyo, Suma Lee alishawahi kutamba na nyimbo zake kama ‘Hakunaga’, ‘Utanikumbuka’, ‘Chungwa’ na nyinginezo ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri katika tasnia ya muziki wa bongo fleva.

No comments:

Post a Comment

Pages