Na Elizabeth John
NYOTA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ismail
Seif ‘Suma Lee’ ameachia kibao chake kipya kinachokwenda kwa jina la ‘Hawa’
ikiwa ni mfululizo wa kuwapa burudani mashabiki wake.
Akizungumza na Habari Mseto jijini Dar es
Salaam, Suma Lee alisema anamshukuru mungu kibao hicho kimepokelewa vizuri na
mashabiki wake na kwamba waendelee kumapa sapoti katika kazi zake.
Suma Lee alisema yupo katika hatua za mwisho za
uandaaji wa video ya kazi hiyo ambayo anaamini itafanya vizuri kutokana na
maandalizi mazuri pamoja na mazingira ambayo ameyafanyia kazi.
“Namshukuru mungu kazi zangu huwa zinapokelewa
vizuri na mashabiki wangu, kitu ambacho kinanipa matumaini ya kuendelea kutunga
mashairi ambayo yatakuwa na mvuto kwa mashabiki wangu,” alisema Suma Lee.
Suma Lee alishawahi kutamba na vibao vyake kama,
Chungwa, Hakunaga, utanikumbuka na nyinginezo ambazo zilimtambulisha na kufanya
vizuri katika vituo mbalimbali vya redio.
No comments:
Post a Comment