HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 10, 2013

UTEUZI WA RAIS UTAUA DEMOKRASIA

Mratibu wa Mtandao wa Mashirika yasiyo ya kiserikali Arusha  (ANGONET), Peter Ahham akifafanua jambo juu ya tamko la Asasi za kiraia Arusha kuhusu Mchakato wa kuandika Katiba Mpya ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania lilokuwa likizungumzia rasilimali pamoja na masuala ya ardhi,katikati ni Mweka Hazina wa Angonet  Bi.Jovita Mlay na wakwanza kulia ni Katibu Mtendaji wa ANGONET, Peter Bayo.Picha na Ferdinand Shayo.

Na Ferdinand Shayo, Arusha

Mratibu wa Mtandao wa Asasi za Kiraia  mkoani Arusha (ANGONET)  Bwana Petro Ahham amesema kuwa uteuzi wa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuteua wajumbe 166 wanaowakilisha makundi mbali mbali ya kijamii katika Bunge Maalum la Katiba utaua demkokrasia hivyo amemtaka Raisi  Kikwete kutoa fursa kwa makundi hayo kuchagua wawakilishi wao.

Aidha amesema kuwa hatua hiyo ni katika kujenga msingi wa demokrasia na uwakilishi wenye maana endapo makundi hayo yatapata nafasi ya kujichagulia wajumbe wao.
Kwa mujibu wa kifungu cha 22 (1) cha sheria ya mabadiliko ya Katiba,Bunge Maalumu  litakuwa na jumla ya wajumbe 604,yaani Wabunge 357,Wawakilishi 81 na wajumbe  166 wanaowakilisha makundi mbali mbali ya kijamii.

“Uchambuzi unaonyesha kifungu hiki cha sheria kinatoa fursa finyu  ya uwakilishi kwa wadau walio wengi na kumpa Raisi mamlaka ya mwisho ya kuteua Wajumbe 166 wanaowakilisha makundi ya jamii na Taasisi mbali mbali,kutokana na hali hiyo ni wazi kuwa nia na dhamira safi ya kuwezesha upatikanaji wa Katiba imepotea jambo ambalo halikubaliki” Alisema Petro.

Akifafanua tamko la Asasi za kiraia Arusha kuhusu Mchakato wa kuandika katiba lililotolewa kwa Waandishi wa habari  leo.
Mratibu huyo amesema kuwa ili katiba isiwe ya dola iwe ni ya wananchi ni vyema Rais  akatoa fursa kwa makundi maalumu kuchagua wawakilishi wao.

Akisoma tamko hilo kwa Waandishi wa habari Bi.Jovita Mlay ambaye ni Mweka Hazina wa ANGONET amesema kuwa  wao kama Asasi za kiraia wanaona sio vyema na busara Rais kuteua wawakilishi 166 wa Asasi zisizo za kiserikali na makundi mengine nane kama yalivyoainishwa katika kifungu cha 22 kwa kuwa wanaamini asasi za kiraia na makundi mengine yanaweza kufanya hivyo na kumpata wanaemwamini  kuwawakilisha.
“Asasi za kiraia katika Mkoa wa Arusha kwa ujumla,tungetaka kuona mabadiliko chanya ya Muswada wa Marekebisho ya Sheria yatakayoboresha sheria ya Mabadiliko ya katiba” Alisema Bi.Jovita
Pia wameelezea hofu yao juu ya upigaji katika Bunge maalumu  la katiba kuwa na msukumo unaoegemea zaidi hisia na itikadi za vyama kuliko katiba ya nchi kutokana na sheria ya Mabadiliko ya katiba kuruhusu Wabunge wote wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi,Zanzibar na Wajumbe wa Bunge Maalumu  ambao ni zaidi ya theluthi mbili ambao ni nyingi hivyo kugubikwa na hisia za itikadi za vyama.
“Sisi tunapendekeza kuwa theluthi moja itokane na Wabunge/wawakilishi,nyingine itokane na AZAKI na theluthi ya mwisho iwe imetokana na umma kwa ujumla wake” Alisema Bi.Jovita akisoma tamko hilo

No comments:

Post a Comment

Pages