Na Mwandishi Wetu, Tanga
TIMU ya Coastal Union imeanza maandalizi kabambe ya kuhakikisha inajipanga vema ili kuhakikisha timu hiyo inapata pointi tatu muhimu kwenye mechi yake ya Ligi kuu dhidi ya JKT Ruvu itakayochezwa Jumamosi wiki hii kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani kutokana na umahiri wa kikosi cha timu hiyo.
Akizungumza leo mara baada ya kumalizika mazoezi ya timu hiyo
yanayoendelea kwenye viwanja vya shule ya sekondari Popatlaly, Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema mapungufu yaliyojitokeza kwenye mchezo wao dhidi ya Tanzania Prison tayari Kocha wao mkuu Mkenya James Nandwa alikwisha kuyafanyia kazi na sasa kikosi kipo kamili kuwavaa maafande hao.
Amesema kuwa mchezo huo utakuwa ni mzuri kwa sababu tayari, Kocha Mkuu wa timu hiyo,Mkenya James Nandwa alikwisha fanyia kazi kubwa ya kukiandaa timu hiyo na ataingia kwenye mechi hiyo akiwa na lengo moja la kuhakikisha ushindi unapatikana ili kuweza kusogea kwenye nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara.
Hata hivyo amesema hakuna mchezaji hata mmoja ambaye ni majeruhi na kuwataka wapenzi na mashabiki kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kwenye mechi hiyo itakayochezwa kwenye uwanja wao wa nyumbani.
No comments:
Post a Comment