Na
Bryceson Mathias, aliyekuwa Njombe
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA), Mkoa wa Njombe, Ally Mhagama (Dkt. Sagasaga), ametema
cheche akisema, “Sitahudhuria Vikao vya Mkuu wa Mkoa Dkt. Rehema Nchimbi, iwapo
ataendelea kujinadi, kama Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Vikao vya
Maendeleo ya ‘Njombe tunayoitaka’.
Akizungumza baada ya kususia Kikao cha Nchimbi na Wafanya Biashara, alichoitisha, ili kujadili ‘Njombe tunayoitaka’ katika Ukumbi wa Kyando karibuni, Mhagama alisema, hatahudhuria Vikao vyake, kama atajinadi ni Kada wa CCM wakati ni Rais wa Mkoa.
“Iwapo Wakuu wa Mikoa, Wilaya,
Wakurugenzi na Viongozi wengine serikalini, watajisahau na kuvaa Kofia ya
Serikali na kuitisha Vikao, wakida ni vya Maendeleo ya Kijamii, kumbe ndani
mwake, ni vya Kikada ili kuipigia Debe CCM, Katu Sitahudhuria”.alisema Dkt.
Mhagama.
Mgomo wa Dkt. Mhagama, ulitokana na
Mchango wake kuhusu Hoja ya Dkt. Nchimbi, kupigia Debe kuwa, kuna ajira 6,000
za Wachina zitakazotokana na Uchimbaji wa Madini mkoani humo, hivyo wakazi na
hasa wafanya biashara Njombe, Walime Matunda kwa Wingi ili kuwauzia.
Mhagama alipinga Hoja hiyo akisema,
alitarajia Serikali ya Mkoa itoe Dira kwa Serikali Kuu, iainishe ni Ajira Kiasi
gani, 200 au 300, zitakazotengwa kwa wakazi hao, badala ya wao kuzunguka kwenye
hiyo Migodi wakiuza Mapera na Machungwa kama watumwa, huku Wageni wakifaidi.
Licha ya Nchimbi kumpongeza, ila amechangia
kwa Maneno Makali, alijikwaa kwa kuchomekea kauli kuwa, yeye (Nchimbi) ni mmoja
wa Makada wa CCM, na hapo Mhagama, alisusia Kikao hicho na kusema si cha
Maendeleo ya Njombe, bali ni cha kui-Imarisha CCM au kuidumaza Chadema.
Hata hivyo, baadhi ya Wafanya
biashara waliohojiwa walisema, hawakuona Mashiko ya Kikao hicho, na
wakampongeza Mwenyekiti huyo wa Chadema (Mhagama), kwa Mchango wa kuwatetea
kuwa, wafanyabiashara wamekuwa wakigandamizwa wakirundikiwa Kodi nyingi, hivyo
kikao hicho kilitakiwa kijadili unafuu, si kuwalaghai.




No comments:
Post a Comment