Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatifa, Bernard Membe akimkabidhi tuzo ya heshima ya kujitolea kwa ajili ya madrasa hapa Tanzania, hajjat Tatu Kazuga wakati wa tamasha la kwanza la Qaswida lililofanyika jijini Dar es Salaam na kudhaminiwa na Kampuni ya Dira ya Mtanzania. (Picha na Francis Dande)
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatifa, Bernard Membe akimkabidhi Sheikh Ismail Mohamed tuzo ya heshima katika shughuli na masuala ya Qaswida hapa Tanzania.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatifa, Bernard Membe akimkabidhi Bi. Shamim Khan tuzo ya heshima ya kujishughulisha na kazi za kijamii hapa Tanzania.
Sheikh Ismail Mohamed akizungumza waati wa tamasha la kwanza la Qaswida lililofanyika jijini Dar es Salaam na kudhaminiwa na Kampuni ya Dira ya Mtanzania.
Baadhi wa waumini waliohudhuria tamasha hilo.
Washiriki wa tamasha hilo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatifa, Bernard Membe akizungumza katika tamasha hilo.
Waimbaji
wa Kaswida kutoka kikundi cha Muumini cha Buguruni jijini Dar es Salaam
wakiimba kwenye tamasha la kwanza la Kaswida lililofanyika katika viwanja vya
Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa. Tamasha hilo lilidhaminiwa na
Kampuni ya Dira ya Mtanzania.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akipokea tuzo maalumu
kutoka kwa Sheikh Ismail Mohamed wakati wa tamasha la kwanza la Kaswida lililofanyika
katika viwanja vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa na kudhaminiwa na Kampuni
ya Dira ya Mtanzania.
NA ZAWADI CHOGOGWE
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amewataka Watanzania
kusubiri kwa hamu siku ya kutangaza nia ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu
wa mwaka huu.
Membe alitoa wito huo leo jijini Dar es Salaam katika
Tamasha la Qaswida lililofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya
Benjamini Mkapa.
Alisema siku hiyo ya Juni 6, wananchi wasikilize
nini anataka kuifanya nchi iweze kuondoka ilipo ikiwemo kuendelea kudumisha amani
na utulivu uliopo.
“Mkae tayari siku hiyo, naamini uongozi mzuri wa
nchi ni ule wa kudumisha amani na utulivu na ili nchi iweze kusonga mbele, maadili
kwa viongozi alisema,” alisema Waziri Membe
Pia Membe alitumia nafasi hiyo kuwasihi Watanzania
kuacha kuchagua viongozi ambao kwa nje, wanajinadi wana dini, lakini matendo hayaendani na
maadili ya dini zao.
Alisema ili mtu aweze kuaminika kuwa ana dini,
jamii ifuatilie katika madhehebu yao, hivyo amewasihi wasichague viongozi wanaosaka
uongozi kwa kutoa rushwa.
“Msikubali kuwa na viongozi ambao kwa nje, wanaojinadi
kuwa na dini kinyume na matendo yao, lazima mchague wenye hofu ya Mungu ambayo
husisitizwa na dini zote,”
Alisema uongozi wa heshima ni ule unaochukia
rushwa ambayo ni adui wa haki, hivyo amewataka wananchi kuwaogopa wapenda
rushwa kama ukoma.
Kuhusu tamasha hilo, Waziri Membe alipongeza
uwepo wake ambapo ni kuwalea vijana katika maadili mema ya kumjua Mungu na
kusema anajivunia Taasisi za aina hiyo.
Tamasha hilo lililodhaminiwa na Kampuni ya Dira
Mtanzania chini ya Mkurugenzi wake Alex Msama, zaidi ya vikundi 50 vimeshiriki
tukio hilo la aina yake.
Akizungumza katika Tamasha hilo, Mkurugenzi wa
Ulamaa Promotion Center ya jijini Dar es Salaam, Jumanne Ligopora, alihimiza
umuhimu wa kila mtu kuwa sehemu ya ulinzi wa amani na utulivu.
Katika hatua nyingine, watu mbalimbali walipewa
tuzo katika tamasha hilo akiwemo Waziri Membe kutokana na mchango wake katika
masuala ya kijamii.
No comments:
Post a Comment