HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 03, 2018

NMB yaitambia CRDB ‘Bankers Basketball League’

 Wachezaji wa timu za kikapu za NMB (jezi ya orange) na wa CRDB wakiwania mpira wakati wa pambano la mpira wa kikapu la Michuano ya Mabenki (Bankers Basketball League - BBL 2018) uliofanyika Jumamosi kweenye Viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam. NMB ilishinda kwa vikapu 52-42.
Wachezaji wa timu za kikapu za NMB (jezi ya orange) na wa CRDB wakiwania mpira .
Mchezaji wa timu ya kikapu ya NMB, akiwatoka nyota wa timu ya CRDB, wakati wa pambano la mpira wa kikapu la Michuano ya Mabenki (Bankers Basketball League - BBL 2018) uliofanyika Jumamosi kweenye Viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam. NMB ilishinda kwa vikapu 52-42.
 Mchezaji wa NMB, Danford, akimiliki mpira uku akizongwa na Johnson Ching wa CRDB.
 Mchezaji wa timu ya kikapu ya NMB, akiruka juu kufunga dhidi ya timu ya CRDB, wakati wa pambano la mpira wa kikapu la Michuano ya Mabenki (Bankers Basketball League - BBL 2018) uliofanyika Jumamosi kweenye Viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam. NMB ilishinda kwa vikapu 52-42.

Mchezaji wa timu ya mpira wa kikapu ya Benki ya CRDB, Godwin Semunyu,  akijaribu kumzuia mchezaji wa NMB.
Mchezaji wa timu ya mpira wa kikapu ya Benki ya CRDB, Johnson Ching, akimtoka mchezaji wa NMB, Danford wakati wa Michuano ya Mabenki (Bankers Basketball League-BBL 2018) uliofanyika kwenye Viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. NMB ilishinda kwa vikapu 52-42. (Picha na Francis Dande).
Mchezaji wa timu ya mpira wa kikapu ya Benki ya CRDB, Godwin Semunyu, akimtoka mchezaji wa timu ya NMB wakati wa Michuano ya Mabenki (Bankers Basketball League-BBL 2018) uliofanyika kwenye Viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. NMB ilishinda kwa vikapu 52-42. (Picha na Francis Dande).

NA SALUM MKANDEMBA

MICHUANO ya Mabenki kwa Mpira wa Kikapu (Bankers Basketball League – BBL 2018), imezidi kushika kasi, ambako mwishoni mwa wiki kikosi cha Benki ya NMB kiliigaragaza timu ya CRDB kwa jumla ya vikapu 52-42.

NMB chini ya Kocha Mkuu Evarist Mapunda, ilitawala kwa kiasi kikubwa pambano hilo, lililofanyika kwenye Viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam, ambako walimaliza nusu ya kwanza ya mtifuano huo wakiwa mbele kwa vikapu 26-15.

Katika nusu ya pili, kujimiani kulikopitiliza kuliwafanya nyota wa NMB kupunguza kasi, ambako walijikuta wakiimaliza nusu hiyo hiyo kwa kipigo cha vikapu 27-26, ingawa havikutosha kuwapa CRDB ushindi wa jumla, hivyo NMB kushinda 52-42.

Akizungumza baada ya mchezo, Kocha wa NMB, Mapunda, aliwapongeza nyota wake kwa upambanaji uliofanikisha kuibuka na ushindi huo na kwamba wamejipanga kuhakikisha wanautwaa ubingwa wa michuano hiyo inayofanyika kila mwaka.

“Tumetimiza lengo la kuibuka na ushindi katika mechi dhidi ya CRDB, nawaponeza nyota wangu kwa upambanaji na sasa tunaelekea kwenye mazoezi kujiandaa na mechi zijazo kulingana na ratiba, ili kufanikisha lengo kuu la kutwaa ubingwa,” alisema Mapunda.

Kabla ya NMB kuichachafya CRDB, pambano la awali juzi lilizikutanisha DTB na TADB, ambako kikosi cha DTB kiliibuka na ushindi wa vikapu 73-40, ambako washindi waliongoza kwa vikapu 40-16 katika nusu ya kwanza, kisha 33-24 katika nusu ya pili.

Bankers Basketball League 2018 ilianza kutimua vumbi Oktoba 27 mwaka huu katika Viwanja vya Gymkhana, Ocean Road jijini Dar es Salaam, ikishirikisha benki mbalimbali nchini zikiongozwa na NMB.

No comments:

Post a Comment

Pages