Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa Rejareja wa Benki ya I&M, Ndabu Swere, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati wa kutangaza washindi wa droo ya kwanza ya ‘Jidabo na I&M Bank’ iliyoanza Oktoba 1 hadi Desemba 31. (Picha na Francis Dande).
Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa Rejareja wa Benki ya I&M, Ndabu Swere.
Baadhi ya Maofisa wa I&M Bank.
Washindi wakitangazwa.
NA MWANDISHI WETU
HATIMAYE
washindi watano wa Promosheni ya ‘JIDABO na I&M Bank,’ wamepatikana
baada ya droo ya kwanza ya shindano hilo kuchezeshwa chini ya wasimamizi kutoka
Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT).
‘JIDABO
na I&M Bank’, ni promosheni inayoendeshwa na I&M Bank, ambayo
inawawezesha wateja wenye akaunti yenye akiba inayoanzia Sh. 200,000, huweza
kujishindia kiasi cha pesa mara mbili ya akiba yake isiyozidi Sh. Milioni 5.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa Rejareja wa I&M Bank,
Ndabu Lilian Swere, alisema washindi watano waliopatikana jana ni sehemu ya
washindi 15 ambao watapatikana katika kipindi chote cha miezi 3 ya ‘JIDABO na
I&M.’
“IIi
kushiriki JIDABO na Bank I&M, unapaswa kufungua Akaunti ya Akiba, Akaunti
ya Biashara, Akaunti ya Mshahara au Akaunti ya Mtoto katika tawi lolote la benki
yetu kuanzia Oktoba Mosi mwaka huu hadi Desemba 31,” alisema Swere.
Aliongeza
kuwa, kwa mteja ambaye tayari ana akaunti ya Benki ya I&M, anapaswa
kuhakikisha kuwa ana akiba ya Tsh. 200,000, ikiwa anamiliki Akaunti ya Biashara
(Current Account) au Tsh. 100,000 ikiwa anamiliki akaunti nyingine zinazohusika
katika promosheni.
Washindi
watano waliopatikana katika droo hiyo ya kwanza ya ‘JIDABO na I&M Bank,’
iliyosimamiwa na Chiku Saleh kutoka GBT ni Selcom Wireless Ltd, Jumanne Francis
Mchench, Eliakunda Emmanuel Shoo, Sherbanu Osman na Eco Dry Cleaners Ltd.
Kwa
mujibu wa promosheni hiyo, washindi hao watano watapata mara mbili ya akiba
zilizopo kwenye akaunti zao, ambapo kiwango cha juu zaidi kutolewa kwa mteja
kitakuwa Sh. 5,000,000/=.
Swere
alifafanua ya kwamba, ikiwa akiba ya mwezi husika ya mteja ni Sh. Mil. 5, basi
itazidishwa mara mbili na kuwa Sh. Mil. 10, na kwamba endapo akiba ya mwezi ya
mteja ikizidishwa mara mbili ya kiasi ambacho anatakiwa kuongezewa mteja ili
kufika mara mbili ya akiba yake kitazidi Sh. Mil. 5, basi mteja atapewa Sh.
Mil. 5 na si zaidi ya hapo.
“Tunawakaribisha
Watanzania wote kuchangamkia fursa hii na kufungua akaunti katika matawi yetu kwenye
mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha na Moshi Mkoani Kilimanjaro, ili waweze
kujidabo na Benki ya I&M na kufanikisha mipango yao mbalimbali iliyobaki
kuelekea mwisho wa mwaka 2018,” alimaliza Swere.




No comments:
Post a Comment