Kurugenzi ya Huduma kwa Umma
kupitia kitengo cha Mafunzo Endelevu kimetoa mafunzo ya siku nne kwa wasaidizi
wa ofisi kuanzia tarehe 8 hadi 11 Oktoba, 2019.
Akizungumza wakati wa
ufunguzi wa mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi Huduma kwa Umma Dk. Arnold Towo
amesema, “wasaidizi wa ofisi hawana budi kufahamu haki na wajibu wa kazi zao
kwa kuzingatia kanuni za Utumishi wa Umma”.
“Kama wasaidizi wa ofisi ni
vema kuzingatia maadili ya Utumishi wa Umma muwapo kazini, kufahamu namna bora
za utoaji wa huduma kwa mteja pamoja na utunzaji wa kumbukumbu na kutunza siri
za ofisi”, alisema Dr. Towo.
Pamoja na hayo Dr. Towo
aliwasisitiza wasaidizi wa Ofisi kuzingatia Utunzaji wa muda, mali na usalama
wa vitu vya ofisi kwa umakini wanapokuwa sehemu zaoza kazi.
Miongoni mwa masuala ya
kuzingatia kazini ni kufanyakazi kwa ushirikiano, kutoruhusu migogoro ambayo
husababisha msongo wa mawazo, alisema Dr. Towo.
Mafunzo hayo ya wasaidizi wa
Ofisi ni kwa ajili ya kuwajengea uwezo na kuwaongezea ujuzi kazini. Mafunzo
hayo yatafungwa rasmi tarehe 11 Oktoba, 2019.
Imetolewa na Afisa Uhusiano
Kurugenzi ya Huduma kwa Umma
Tarehe 8 Oktoba,2019
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Huduma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Zamda Kiula, akizungumza na washiriki kabla ya kuanza kwa mafunzo hayo.
Kaimu Mkurugenzi Kurugenzi ya Huduma kwa Umma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dk. Arnold Towo, akifungua mafunzo ya siku nne kwa wasaidizi
wa ofisi kuanzia tarehe 8 hadi 11 Oktoba, 2019.
Kaimu Mkurugenzi Kurugenzi ya Huduma kwa Umma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dk. Arnold Towo, akifungua mafunzo ya siku nne kwa wasaidizi
wa ofisi kuanzia tarehe 8 hadi 11 Oktoba, 2019.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa.
Baadhi ya washiriki wakiwa katika mafunzo.
Kaimu Mkurugenzi Kurugenzi ya Huduma kwa Umma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dk. Arnold Towo, akifungua mafunzo ya siku nne kwa wasaidizi
wa ofisi kuanzia tarehe 8 hadi 11 Oktoba, 2019.
Mtumishi kutoka Kituo cha Afya, Anna Mwahu, akijitambulisha kabla ya kuanza kwa mafunzo.
Utambulisho.
Shaban Msumi kutoka Ofisi ya Makamu Mkuu wa Chuo akichangia mada katika mafunzo hayo.
Mshiriki.
Mkufunzi
wa Mafunzo ya Wasaidizi wa Ofisi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Peter Mbago, akitoa
mada kuhusu Huduma kwa Wateja.
Washiriki.
No comments:
Post a Comment