Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe (kushoto) akisaini mikataba na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya A. V Consult Arch.Victor Ponera (kulia) kwa ajili ya usanifu na ujenzi wa maghala 14 ya hifadhi mahindi na karanga kudhibiti sumukuvu.
Katibu
Mkuu Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akitoa maelekezo kwa
washauri elekezi waliosaini miradi ya kazi kwa ajili ya kutekeleza mradi
wa Kudhibiti Sumukuvu nchini.Tukio lilifanyika katika ukumbi wa
mikutano wa wizara Mtumba, Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe (kushoto) akibadilishana nyaraka za mashirikiano na Mwanasheria wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Kelvin Rogers. TBS itasaidia kutoa elimu kwa wajasiliamali na Wafanyabiashara kuzalisha na kuhifadhi nafaka kwa kuepuka sumukuvu. (Picha na Habari Wizara ya Kilimo).
Dodoma, Tanzania
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mhandisi
Mathew Mtigumwe amewataka washauri elekezi waliosaini mikataba ya kusanifu
miundombinu kwa ajili ya utekelezaji mradi
wa kudhibiti Sumukuvu (TANIPAC) kuifanya kazi hiyo kwa weledi na ubora.
Ametoa kauli hiyo jana Jijini Dodoma wakati wa hafla ya kusaini mikataba
mitatu na Makampuni yenye thamani ya Shilingi Milioni 868.7 ,randama mbili za
mashirikiano na taasisi za TBS na VETA
kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa kudhibiti Sumukuvu nchini.
“Mfanye kazi kwa weledi sana, sasa
Wizara ya Kilimo tunazingatia weledi.Hatutamvumilia mshauri elekezi mzembe
,tutawasimamia kwa karibu na kuhakikisha thamani ya fedha inaonekana kwenye
miradi hii ya kudhibiti sumukuvu” alisema Mhandisi Mtigumwe.
Kampuni zilizo saini mikataba ni M/S
Digital Space kusanifu karantine ya maabara ya utafiti wa magonjwa ya
kibaiolojia,Sundy Merchant Ltd kufanya tahthmini ya awali ya mradi wa Sumukuvu
na A.V Consult kufanya usanifu na ujenzi wa maghala 14 ya hifadhi ya mahindi na
karanga.
Aidha, Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Stadi (VETA) imesaini randama ya mashirikiano ya kufundisha vijana mafundi
mchundo 400 kutengeneza teknolojia ya kuhifadhi mazao wakati Shirika la Viwango
(TBS) limeingia makubaliano na Wizara ya Kilimo kusaidia kutoa elimu kwa
wajasiliamali na Wafanyabiashara kuzalisha na kuhifadhi mazao kwa kuepuka
sumukuvu ili wapate soko la uhakika na salama katika mnyororo wa thamani ya
mazao nchini.
Akizungumza wakati wa utiaji saini
Mkurugenzi Mkuu wa VETA nchini Dkt. Pancras Bujulu alisema ni fursa nzuri
wamepata kufundisha mafundi mchundo kutengeneza vihenge rahisi kwa ajili ya
kuhifadhi mazao ya wakulima ili kulinda afya za watu kwa kutumia teknolojia
bora
“Ni
wajibu wetu VETA kutoa mafunzo kwa vijana nchini ili wazalishe vifaa bora
(vihenge) kwa ajili ya kuhifadhi nafaka na kujipatia ajira” Dkt. Bujulu alisema.
Aliongeza kusema vijana hawa 400 toka
wilaya 18 za Tanzania Bara watakuwa chachu ya kusambaza teknolojia hii rahisi
na bora ya uhifadhi nafaka nchini.
Mratibu wa mradi wa kudhibiti Sumukuvu
(Tanzania Iniatives for Preventing Aflatoxin Contamination-TANIPAC) Clepin
Josephat alisema mradi huu wa miaka mitano(2019-2023) unatekelezwa nchini kwa
lengo la kuhakikisha usalama wa chakula hususan kwenye mazao ya mahindi na
karanga hayachafuliwi na fangasi wanaosababisha sumukuvu.
Aliongeza kusema sumukuvu tangu
ilipogunduliwa nchini imesababisha madhara kwa wananchi ikiwemo kuongezeka kwa
uwezekano wa kansa ya ini,udumavu kwa watoto chini ya miaka 5 na vifo.
Katika mwaka 2016 jumla ya watu 19
walikufa na wengine 68 waliugua na
kulazwa kutokana na sumukuvu aina ya Aflatoxin kwenye mikoa ya Dodoma na
Manyara ambayo imeathirika zaidi.
No comments:
Post a Comment