HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 10, 2020

Mikoa saba kupata mvua kubwa leo, kesho - TMA


Na Irene Mark

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetoa angalizo la kuwepo kwa siku mbili za mvua kubwa kwenye mikoa saba kuanzia leo Januari 10,2020.

Mikoa itakayopata mvua hizo kwenye baadhi ya maeneo ni Singida, Rukwa, Mbeya, Iringa, Njombe, Songwe na Dodoma.

Akizungumza na Habari Mseto Blog, Meneja wa Utabiri kutoka Kituo Kikuu cha Utabiri TMA, Samuel Mbuya alisema mvua hizo zitaanza leo hivyo kuwataka wakazi wa mikoa hiyo kuchukua tahadhari.

"Ni vema watu wakachukua tahadhari ikiwemo kuzibua mifereji ili kuruhusu maji yasituame sehemu moja maana hiyo ndio chanzo cha mafuriko lakini pia kuhakikisha wanawahi kwenda kwenye maeneo yao ya kazi na kuondoa msongamano barabarani," alisema Mbuya.

Kwa mujibu wa meneja huyo mamlaka itaendelea kutoa tahadhari, angalizo na taarifa mbalimbali za hali ya hewa kwa wananchi ili kuwakinga na majanga yanayoweza kutokea kwenye jamii.

No comments:

Post a Comment

Pages