Mbunge
wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo
ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kulia akigawa msaada wa
moja ya kumpyuta 20 kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari kulia leo
ambapo shule 10 zitanufaika na msaada huo ambao umetolewa na Tume
ya Mawasiliano nchini wenye thamani ya milioni 16.
Mbunge
wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo
ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kulia akigawa msaada wa
moja ya kumpyuta 20 kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Mnyanjani
Saida Mahadhi kushoto ambapo shule 10 zitanufaika na msaada huo ambao umetolewa na Tume
ya Mawasiliano nchini wenye thamani ya milioni 16 kulia ni Mwenyekiti
wa CCM wilaya ya Tanga Meja Msaafu wa Jeshi Mkoba
Mbunge
wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo
ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kulia akigawa msaada wa
moja ya kumpyuta 20 kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari kulia leo
ambapo shule 10 zitanufaika na msaada huo ambao umetolewa na Tume
ya Mawasiliano nchini wenye thamani ya milioni 16 katikati mwenye miwani
ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji na kushoto Mwenye Kaunda
suti ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa.
MBUNGE
wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) ambaye pia ni Waziri wa Afya
Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza
wakati wa halfa ya makabidhiano hayo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga
Thobias Mwilapwa.
Mkuu
wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa halfa hiyo
kushoto ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) ambaye pia ni
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na
kulia ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji.
Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji akizungumza wakati wa makabidhiano hayo. |
Afisa Elimu Jiji la Tanga Lusajo Gwakisa akitoa taarifa ya elimu wakati wa makabidhiano hayo.
Sehemu ya wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo walimu wakuu wa shule za sekondari na wadau wakifuatilia makabidhiano hayo.Sehemu ya walimu wa shule ya Sekondari Mkwakwani wakifuatilia makabidhiano hayo.
Sehemu ya Kompyuta 20 zilizotolewa na Waziri wa Afya Maendelelo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) kwa shule 10 za sekondari Jijini Tanga.
Na Mwandishi Wetu
MBUNGE
wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa wa Afya Maendeleo ya
Jamii Ummy Mwalimu leo ametoa msaada wa kompyuta 20 kwa shule 10 za Sekondari
Jijini Tanga ili kutoa fursa kwa wanafunzi kusoma somo hilo kwa vitendo
ikiwemo kusaidia utendaji wa kazi wao.
Makabidhiano hayo yalifanyika leo kwenye shule ya Sekondari Mkwakwani Jijini Tanga kwa niaba ya shule zote ambazo zitanufaika na msaada huo ambao umetolewa na Tume ya Mawasiliano nchini wenye thamani ya milioni 16.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo Mbunge Ummy alisema kwamba ametoa kumpyuta hizo sio wanafunzi watumie kucheza karata bali ni kurahisisha bajeti za shule katika n gazi ya shule, uandaaji wa malipo kwa kutumia mfumo wa FFARS.
“Lakini pia zitasaidia usajili wa wanafunzi na usajili wa watahiniwa vyote vitasaidia hivyo Mkurugenzi wa Jiji Daudi Mayeji wasaidia WIFI kwa lengo la kurahisisha baadhi ya mambo yanayohitajika kutumia mtandao”Alisema
Mbunge huyo alisema kwamba kwa shule ambazo hazijapata msaada huo atakwenda kutafuta lengo lake ni kutafuta vishkwabi kwa ajili ya wanafunzi kuhakikisha wanasoma somo la kompyuta huku akihaidi pia kujengwa vyumba vitano vya madarasa
“Niwashukuru lakini niendelee kuwaomba wanafunzi fanyeni kazi kwa kujitumua na tunatambua vipi changamoto za walimu tutaendelea kuzipatia ufuimbuzi”Alisema
Hata hivyo amehaidi kwamba ataendelea kuwasemea wananchi wa Jiji la Tanga kwa kutumia nafasi yake kuhakikisha maslahi ya walimu yanakuwa mazuri.
Awali akizungumza katika makabidhiano hayo Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa alisifu juhudi zinazofanywa na Mbunge Ummy kuhakikisha anawasaidia wananchi wa Jiji la Tanga kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya elimu.

Alimpongeza Waziri Ummy kwa msaada huo ambao amewapatia shule hizo kwani miongoni mwao ni zile ambazo zinaupungufu wa madarasa zimenufaika na msaada huo wa kompyuta.
Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji alisema kwamba msaada huo wa komputa utakuwa chachu kubwa kwao kwani serikali ya sasa imefanya mageuzi makubwa.
Alisema kutokana na mageuzi hayo hakuna malipo yanayoweza kufanyika bila mfumo kwa hiyo msaada huo wa kumpyuta 20 shule hizo zitakuwa zimeondolewa kwenye tatizo la kutokuweza kufanya malipo kutumia mfumo.
“Kutokana
na kwamba shule nyingi au Taasis zimekuwa zikienda shule za jirani
kutokana wengi kutokuwa nazo hivyo msaada huo utakuwa chachu kubwa kwa
kuongeza ufanisi katika utendaji wao “Alisema.
Awali
akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Afisa Elimu Jiji la Tanga
Lusajo Gwakisa alimshukuru Mbunge Ummy kwa msaada huo wa kompyuta 20
utakwenda kupunguza upungufu uliopo wa Kompyuta bali italeta tija katika
maendeleo.
“Maendeleo
hayo ambayo msaada huu utaleta tija ni utayarishaji wa bajeti katika
ngazi za shule lakini pia uandaaji wa malipo kwa kutumia mfumo wa FFARE
pamoja na usajili wa wanafunzi wanaoanza kidato cha kwanza “Alisema
Hata hivyo alisema kwamba pia vitasaidia uhamishaji wa taarifa za wanafunzi kwa kutumia mfumo wa PREM ikiwemo usajili wa watahiniwa wa kidato cha pili,nne na sita na kutunza kumbukumbu nyengine za utawala.

No comments:
Post a Comment