Mgeni rasmi kwenye kufunga mashindano hayo ya Wafanyakazi wa SUA Bi. Asteria Mwang'ombe ambaye ni Afisa Michezo wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro akipata maelekezo kwa waamuzi wa mchezo huo wa mpira wa miguu.
Na Calvin Gwabara
WATANZANIA wametakiwa kuhakikisha wanatenga muda kwa ajili ya kushiriki kwenye michezo na
mazoezi mbalimbali ya mwili ili kusaidia kujenga mwili na taifa la watu wenye
afya watakaoleta maendeleo.
Wito huo
umetolewa na Afisa Michezo Manispaa ya Morogoro Bi Asteria Mwang’ombe kwa niaba
ya mkurugenzi wa manispaa hiyo wakati akizungumza na wanamichezo na wanajumuiya
wa SUA, Benki ya CRDB na NMB wakati akifunga rasmi michezo kwa ya wafanyakazi
wa SUA ya Chibunda CUP.
Bi. Asteria
ameupongeza uongozi wa SUA kwa kuamua kuanzisha michezo hiyo ambayo
inawakutanisha wafanyakazi wote wa SUA kwenye michezo 20 mbalimbali na
kuipongeza benk ya NMB kwa kuamua kufadhili mashinano hayo kila mwaka toka
kuanza kwake.
‘’ Naupongeza
sana uongozi wa SUA kwa kulipatia kipaumbele swala la michezo kwa wafanyakazi
na wanafunzi hasa kwa kuamua kuanzisha idara maalumu kwaajili ya michezo Chuoni
hii ni hatua nzuri kwani itaongeza ufanisi na ari ya wanajumuiya wa SUA
kushiriki kwenye michezo” Alisistiza Bi. Asteria.
Afisa
michezo huyo ameahidi kutoa ushirikiano wowote utakaohitajika katika
kufanikisha michezo chuoni hapo ikiwemo swala la walimu wamichezo pale
watakapohitajika na kwamba changamoto mbalimbali zilizobainishwa atazifikisha
kwa uongozi wa manispaa ili kuona namna ya kuzitatua.
Akizungumza
kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kufunga maichezo hiyo Naibu makamu mkuu wa
chou upande wa taaluma Prof. Amandus Muhairwa kwa niaba ya makamu mkuu wa chou
Prof. Rapgael Chibubda amesema michezo hiyo ni sehemu ya Chuo kupata
wanamichezo ambao watakiwakilisha chou kwenye michezo mbalimbali ndani nan je
ya nchi.
Prof.
Muhairwa amesema Uongozi wa chou unathamini sana umuhimu wa michezo ndio maana
imeweka mikakati mbalimbali ya kuboresha viwanja na kununua vifaa mbalimbali
vya michezo kwenye kampasi zake zote ili wafanyakazi na wanafunzi washiriki
vyema michezo.
‘’ Kutokana
na idadi kuwa ya wanafunzi na wafanyakazi Chuo kinaendelea na jitihada za
kuongeza viwanja vipya na vya kisasa ili kukidhi mahitaji na tayari kiwanja
kipya cha mchezo wa kikapu cha kisasa Mkoani Morogoro tumemaliza kukijenga na
sasa kinatumika hat ana watu wan je ya Chuo” alifafanua Prof. Mhairwa.
Hata hivyo
ametumia nafasi hiyo kuupongeza uongozi wa benki ya NMB kwa kufadhili
mashindano hayo ya wafanyakazi kwa miaka minne mfululizo lakini akaomba wadau
kuwaunga mkono kwa kujitokeza kufadhili mashindano ya wanafunzi ili ambayo ni
mikubwa na yenye mvuto sana.
Kwa upande
wake Muwakilishi wa banki ya CRDB Bi. Isabela Kitila ambaye ni meneja wa tawi
la CRDB SUA ameshukuru uongozi wa SUA kwa kuendelea kuwashirikisha katika
michezo hii kwa miaka minne mfululizo kama wadhamini wakuu na kuahidi kuendelea
kudhamini kila mwaka.
Isabela
amesema kuwa michezo hiyo imewafanya wana CRDB na wanajumuiya wa SUA kuishi
kama ndugu na familia kwakuwa michezo imekuwa ikiwaunganisha kwa njia
mbalimbali na kufahamiana ikizingatiwa idadi kubwa ya wafanyakazi wa SUA
waliopo bila michezo isingekuwa rahisi.
“Niwahakikishie
kuwa sisi kama CRDB mlipo tupo na tutaendelea kuwepo katikati yenu kwenye
kushiriki michezo hii na mambo mengine hivyo karibuni sana kwenye benki yetu
muweze kupata huduma pia za kibenki mbalimbali kulingana na mahitaji yenu maana
sisi na nyinyi ni familia moja” alisistiza Isabela.
Nae Menejea
wa Benki ya CRDB Tawi la Wami Bw. Harold Lambileki amesema ndio mara
ya kwanza kushiriki kwenye michezo hiyo hivyo wamekuja kujifunza kuona
kinachofanyika ili na wao waweze kushiriki kikamilifu kama wadau muhimu wa
michezo nchini.
Amesema
Wanamichezo ndio wateja wa huduma za benki hiyo watahakikisha kwenye
michezo ijayo nao wanakuwa sehemu ya wadhamini wa michezo hiyo muhimu ya
wafanyakazi lakini pia kwenye michezo mingine ili kusaidia kuboresha afya na
kuimarisha undug una ushirkiano.
Michezo hiyo ya wafanyakazi wa SUA ilianza miaka minne iliyopita na imekuwa ikishidanisha wafanyakazi wote kwenye michezo mbalimbali 20 na mwisho wa michezo hiyuo zawadi mbalimbali zinatolewa ikiwemo vikombe,medali na fedha taslimu wa washindi.
No comments:
Post a Comment