HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 08, 2021

UTT AMIS YATOA SEMINA KWA WABUNGE, WATUMISHI KUHUSU UWEKEZAJI WA PAMOJA

KAMPUNI ya UTT AMIS imetoa semina kwa Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na watumishi wake iliyofanyika jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.
 
Lengo la semina hiyo ikiwa ni kuwapa uelewa wabunge na watumishi kuhusu uwekezaji kwenye mifuko ya uwekezaji wa pamoja.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa UTT, Simon Migangala alisema kuwa Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja inatoa unafuu wa kuwekeza kwenye hatifungani, akaunti za muda maalum na hisa za makampuni yanayofanya vizuri ambapo mwekezaji ana uwezo wa kupata hisa zote ambazo mfuko umewekeza kwa ununuzi mmoja.
 

Kwa upande wake Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai, aliupongeza mfuko huo kwa kuandaa semina hiyo ambayo imetoa fursa kwa wabunge na watumishi kupata elimu juu ya Uwekezaji Wa Pamoja. "Kuna faida kubwa ambazo mtu anaweza kupata kwa kuwekeza katika mifuko inayosimamiwa na UTT AMIS". Alisema Spika Ndugai.

Mifuko ya uwekezaji wa pamoja inaratibiwa na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na inadhibitiwa na sheria ya mifuko ya uwekezaji wa pamoja yenye lengo la kumlinda mwekezaji. Kanuni hizi zinahusiana na shughuli za kampuni za Usimamizi/Uwendeshaji wa mifuko ya uwekezaji wa pamoja. 

 
Mkurugenzi Mtendaji wa UTT, Simon Migangala, akitoa elimu ya fursa zinazopatikana kwenye mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja kwa wabunge na watumishi wakati wa semina iliyofanyika jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Spika wa Bunge, Job Ndugai akisisitiza juu ya umuhimu wa kuwekeza kwenye mifuko ya uwekezaji ya UTT AMIS.
Spika mstaafu Pius Msekwa akitoa ushuhuda jinsi alivyonufaika na mifuko inayosimamiwa na UTT AMIS.
Mmoja wa wabunge akiuliza swali.

No comments:

Post a Comment

Pages