HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 28, 2022

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo aongoza WILLNESS DAY ya Benki ya CRDB



 Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kheri Jamse akiongoza wafanyakazi wa Benki ya CRDB kupima afya wakati wa Maadhimisho Siku ya Willness Day iliyoandaliwa na benki hiyo Kanda ya Mashariki kwa ajili ya wafanyakazi wake katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. 
Akizungumza katika Maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kheri Jamse ameipongeza Benki ya CRDB kwa kuja na program ya Willness ambayo itasaidia wafanyakazi kujua afya zao, kulinda afya zao na kuzijenga afya zao kupitia mazoezi jambo ambalo litaongeza tija katika kazi zao.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Mashari, Badru Idd, akipima urefu pamoja na uzito wakati wa maadhimisho ya Siku ya Willness Day iliyofanyika katika viwanja vya Chuo cha Dar es Salaam (UDSM) jijini Dar es Salaan, mwishoni mwa wiki. 
Naye Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Mashariki, Badru Idd, amesema kuwa benki hiyo imekaa na kubuni Program ya Wellness Day “tumejaribu kuangalia huyu mfanyakazi anayefanyakazi ndani ya CRDB tutamjengaje kama bidhaa adimu ili aweze kuzalisha vizuri lakini pia ili awe na afya njema.

Alisema kuwa lengo kuwaita wafanyakazi wa benki ya CRDB na kuelezana vizuri ili tuwe na tija, ili akili iwe na afya anatambua magonjwa nyemelezi yanayomzunguka kama presha, sukari tunapokuwa katika viwanja hivio tunawaleta wadau wetu tofauti, madaktari wanatupima tunajua afya zetu na kuchukua tahadhari, lakini pia kufanya mazoezi.

Wafanyaka zaidi ya 700 walishiriki katika maadhimisho hayo kutoka katika matawi 50 ya Benki ya CRDB Kanda ya Mashariki. 

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kheri Jamse (wa pili kulia) akiwaongoza wafanyakazi wa Benki ya CRDB katika Maadhimishi ya Willness Day katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kulia ni Meneja wa CRDB Kanda ya Mashariki, Badru Idd.          


No comments:

Post a Comment

Pages