Meneja wa
Benki ya NMB Kanda ya Kati, Nsolo Mlozi (katikati), akionyesha kadi za benki
ambazo mteja akitumia kwenye manunuzi ataingia kwenye droo ya ‘NMB MastaBata
Kivyakovyako’ ambapo droo ya Mwezi ilichezeshwa Jijini Dodoma. Kulia
ni Afisa Huduma kwa Wateja Benki ya NMB, Suzan Manga na kushoto ni Mwakilishi
kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini , Ibrahim Shikana. (Na Mpigapicha
Wetu).
Benki ya NMB imechezesha Droo ya mwezi wa pili wa MastaBata kivyakovyako jijini Dodoma na kuwazawadia Wateja wao jumla la Tsh Milioni 25.
Tabasamu
la mwanzo wa mwezi limewadodokea Wateja 25 wa NMB ambao kila mmoja
aliibuka na kitita cha Tsh Milioni 1 kutoka kwenye droo hiyo.
Mastabata
kivyakovyako ni droo inayochezeshwa na Benki ya NMB kwa wateja
wanaotumia kadi za Mastercard kwa kufanya malipo kupitia POS au kwa
kuscan QR code na kufanya manunuzi mitandaoni.
Hadi
jana zaidi ya wateja 800 walishajinyakulia kitita cha Sh 100,000 kwa
kila mtu wakaingia droo ya mwezi ambayo imewafikia watu 50 kwa kiwango
na kuondoka na Tsh Milioni 1 kila mmoja, huku wengine 30 wataibuka na
Sh milioni 3 kila mmoja kwa droo ya mwisho.
Meneja
wa Kanda ya Kati wa Benki hiyo Nsolo Mulozi alisema jana kuwa washindi
wa jana walikuwa katika droo ya mwezi ambayo kila mshindi anaondoka na
kitita cha Sh Milioni 1 kwenye shindano lililoanza Desemba 24,2022.
Washindi
wataendelea kuchukua zawadi zao hadi droo ya mwisho ya shindano hilo
ambalo limetengewa Sh 200 milioni na zote zitawafikia wateja.
Afisa
kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Ibrahim Sikana alisema mchezo
huo umekuwa na manufaa kwa wateja na Serikali na kuwa bodi inafurahia
uwepo wake.
Sakana
alisema kwa namna ilivyo, NMB inaweza kuwa moja ya taasisi za kifedha
zinazoaminika zaidi kwenye droo zake kwani hakuna malalamiko yoyote toka
kwa wateja wao.
Wateja
wengi waliokuwa ndani ya benki ya NMB tawi la Dodoma walikusanyanyika
kushudia droo hiyo ambapo wengi walifurahi kuwa ilikuwa imichezeshwa kwa
uwazi na haki.
Mteja
Marius Mazengo alisema hakuwa na taarifa za namna gani huwa wanashinda
lakini alivyotazama jana aliona kuwa mchezo huo ni haki.
Kwa
Kuwa umri wake umekwenda, mara nyingi haji benki anatumia kadi kwa
kukwepa foleni, kwa hiyo kumbe na yeye yupo kwenye orodha ya kushinda na
iko siku najua nami nitashinda- Mazengo.
No comments:
Post a Comment