HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 22, 2022

WANANCHI WATAKIWA KUFUATILIA MIRADI SEKTA YA AFYA SONGEA

  Mratibu wa Mradi wa ufuatiliaji wa matumizi ya rasilimali za umma Dadiely Chanachayo akizungumza wakati wa mafunzo hayo.



 

NA STEPHANO MANGO, SONGEA

 

WANANCHI wametakiwa kufuatilia uibuaji na utekelezaji wa miradi katika sekta ya afya ili waweze kubaini mafanikio na changamoto zake katika ustawi wao kwenye maeneo kusudiwa

Wito huo umetolewa jana na Mratibu wa Mradi wa ufuatiliaji wa matumizi ya rasilimali za umma Dadiely Chanachayo wakati wa mafunzo ya siku tatu ya wajumbe wa PETS kutoka katika kata za Magagura, Litisha na Matimira yaliyofanyika katika ukumbi wa Saccos ya Walimu Songea

Chanachayo alisema kuwa kupitia ufadhiri wa Foundation For Civil Society(FCS) wamedhamiria kuzifikia kata hizo ili kuona mafanikio na changamoto katika utolewaji wa huduma za afya kuanzia ujenzi wa vituo vya afya na Zahanati katika maeneo hayo nakwamba mradi huo utagharimu ruzuku ya shilingi milioni 50.6

Akitoa mafunzo hayo Mshauri Mwelekezi (Consultant) Utawala bora na uwajibikaji Mnung’a Shaib Mnung’a Utawala Bora ni nyenzo muhimu katika Maendeleo ya Nchi, kama ilivyo ainishwa kwa umuhimu wake katika

Mnung’a alisema kuwa Dira ya Taifa 2025,Katiba ya JMT (inayounda Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, ibara 129),Mkukuta I &II Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka 5, ambapo misingi au kanuni za utawala bora ni Demokrasia

Alieleza zaidi kuwa Utawala wa   sheria, uwajibikaji, Haki za binadamu, Uwazi, Maridhiano na ushirikishwaji na kwamba tanzania imejipambanua kama nchi inayofuata Misingi ya Utawala bora kwa kuzingatia misingi ya usawa, uwajibikaji, ushiriki, uwazi, demokrasia na Haki za kijamii.

Alifafanua kuwa hatahivyo, Ushiriki Mpana wa wananchi katika shughuli za Serikali bado ni changamoto ya  kufanyia kazi ndio maana Asasi ya Roa kwa ufadhiri wa Foundation For Civil Society(FCS) wamejikita kuangalia masuala hayo ya utawala bora na uwajibikaji katika mipango ya maendeleo kwenye sekta ya afya

Kwa upande wake mshiriki wa mafunzo hayo kutoka kata ya Matimira Sayuni Komba anasema kuwa mafunzo hayo yatawajengea uwezo katika ufuatiliaji wa mikutano na ujenzi wa miradi kusudiwa.

No comments:

Post a Comment

Pages