Na John Richard Marwa
Matajiri wa Jiji la Dar es Salaam Azam FC leo wanatarajiwa kuvaana na Simba amabyo juzi ilikutana na kichapo kizito cha mabao 3-0 dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, CAFCL huku kocha wa timu hiyo ya Wanalambalamba, Daniel Cadena akinshuhudia Mnyama akilowaa.
Baada ya mchezo huo kocha Cadena unaambiwa alirejea kwenye programu yake ya mazoezi na kuwaongezea wachezaji wake madini ya kwenda kumzimisha tena Mnyama Simba pale pale kwa Mkapa.
Azam watakuwa wageni wa Simba kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara NBC PL, wakiingia na kumbukumbu ya ushindi wa bao 1-0 ilioupata katika mechi ya raundi ya kwanza lililofungwa na Prince Dube.
Habari Mseto ilipata fursa ya kuzungumza na Kocha Cadena amesema kwa namna alivyowatazana Simba anaamini utakuwa mchezo mgumu huku akitaka wachezaji wake kujitoa zaidi ili waweze kupata matokeo.
“Natamani kuona mabadiliko makubwa zaidi kutoka kwa wachezaji kwani tunakutana na timu iliyotoka kupoteza mechi mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL, hawatataka kurudia makosa, wakati nasi tunahitaji zaidi pointi tatu,” amesema Cadena na kuongeza;
“tumekuwa na mazoezi mara mbili asubuhi na jioni lengo lilikuwa kuboresha maeneo yote kuanzia safu ya ulinzi hadi ushambuliaji, sihitaji kuona Azam inakuwa timu ya kuwarudisha wapinzani mchezoni baada ya kutoka kufungwa.” amesema Cadena.
No comments:
Post a Comment