HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 18, 2023

TAIFA STARS IKO TAYARI KUWAVAA NIGER KESHO

Na John Richard Marwa

Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' iko tayari kuwavaa timu ya Taifa ya Niger katika mchezo wa kundi F kuwania kufuzu Afcon 2023, mtanange utakao lindima Dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Hayo yamebainishwa na Kocha msaidizi wa Stars, Hemed Morocco ambaye amesema maandalizi ya kuelekea mchezo huo yamekamilika kwa asilimia 90.

"Tunamchezo muhimu sana hapo kesho, tunahitaji matokeo Ili tuweze kusonga mbele. Niger ni wazuri, tumefanya kazi ya kutazama mazuri yao na madhaifu yao.  Maandalizi yetu yamekamilika kwa asilimia 90.

"Kukosekana kwa Manula ni wazi ni majeruhi anapokosekana yeye waliopo pia ni watanzania nao wanayo nafasi ya kufanya kazi kama ambavyo Manula angekuwepo.

"Maingizo mapya ni mazuri, tumefanya kazi kubwa kuwatazama na kuwaamini na tunaamini ni wachezaji ambao wanakuja kutupatia kile tunachokihitaji leo na baadae."amesema Morocco

Kwa upande wa wachezaji Himid Mao 'Ninja' amesema wanafahamu umuhimu wa mchezo huo huku akiwaita watanzania kwenda kuwasapoti hapo kesho.

"Kwa niaba ya wachezaji tuko tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho, tunafahamu umuhimu wa mchezo huo na tuko tayari lakini tunahitaji sapoti ya mashabiki na kila mtanzania kuja kutoa mchango wake katika huu mchezo." Amesema Himid.

Stars inaingia kwenye mchezo huo ikiwa nafasi ya pili na pointi nne sawa na Uganda walioko nafasi ya tatu, Niger wanabuliza mkia na pointi mbili huku kinara wa kundi ni Algeria mwenyewe pointi 12 na tayari wameshafuzu.

No comments:

Post a Comment

Pages