HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 26, 2023

JKT WANAUME UTAWATAKA LIGI YA TAIFA

Na John Marwa

Timu ya  JKT Wanaume  mpira wa Wavu imeanza kwa kishindo Ligi ya Taifa Mpira wa Wavu Tanzania (TVNL) baada ya kuwachinja Jeshi Stars Seti (3-1).

JKT wameeibuka na ushindi huo jioni ya leo katika viwanja vya Gwambina Lodge zamani TCC CLUB Chang:ombe ukiwa ni mchezo maaluumu wa ufunguzi wa msimu kwa upande wa Wanaume.



Ulikuwa mchezo wa ushindani mkubwa kwa pande zote mbili, licha ya Jeshi Stars kuonyesha ubora wa lakini JKT wameendeleza ubora wao wa kumalizia Seti kama ilivyokuwa kwa timu yao ya Wanawake.

Mchezo huo pia umeonyeshwa mubashara na kituo cha michezo cha Azam Tv kupitia chaneli yao ya Azam Spots 2.

Michezo mingine iliyopogwa mapema ka upande wa Wanaume matokeo ni
NYIKA Seti (3)) vs Nyuki (0), Chui (3) Vs Mafinga (0) huku KIUT (3) VS Mafunzo (1).


Ligi hiyo itaendelea kesho katika Viwanja vya Gwambina ambapo mzunguko wa kwanza utamalizika Juni 30.



No comments:

Post a Comment

Pages