HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 26, 2023

JKT WANAWAKE WAANZA KWA KISHINDO

Na John Marwa

Timu ya  JKT Wanawake  mpira wa Wavu imeanza kwa kishindo Ligi ya Taifa Mpira wa Wavu Tanzania (TVNL) baada ya kuwatwanga Magereza Seti (3-0).

JKT wameeibuka na ushindi huo jioni ya leo katika viwanja vya Gwambina Lodge zamani TCC CLUB Chang:ombe ukiwa ni mchezo maaluumu wa ufunguzi wa msimu kwa upande wa Wanawake.

Ulikuwa mchezo wa ushindani mkubwa kwa pande zote mbili, Magereza walikuwa bora kila mwanzo wa Seti huku JKT wakionyesha ufundi wa kumalizia Seti na uufanikiwa kushinda Seti zote tatu.

Mchezo huo pia umeonyeshwa mubashara na kituo cha michezo cha Azam Tv kupitia chaneli yao ya Azam Sports 2.

Michezo mingine iliyochezwa mapema kwa timu za Wanawake ni Pentagon (1) Vs JKU (3), Korosho Queens (0) Vs Jeshi Stars (3) huku KIUT (3) Vs NHIF (0)


Ligi hiyo itaendelea kesho katika Viwanja vya Gwambina ambapo mzunguko wa kwanza utamalizika Juni 30.


No comments:

Post a Comment

Pages