HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 04, 2023

Kampuni 5000 zashiriki sabasaba

Na Selemani Msuya

KAMPUNI 5666 za ndani na nje ya nchi zimeshiriki kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) maarufu kama Sabasaba yanayofanyika katika Viwanja vya Julius Nyerere jijini hapa.



Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Dk Ashanti Kijaji wakati alipotrembelea maonesho hayo jana ambapo aliweka bayana kuwa idadi hiyo ya washiriki inaonesha namna gani Tanzania ni nchi nzuri kwa uwekezaji na biashara.

“Maonesho haya ya 47 yamekuwa ya mfano wa kuigwa tofauti na miaka mingine iliyopita kwani sasa hivi kampuni nyingi kutoka nje na ndani ya nchi yameshiriki niwaombe wananchi kuja kutembelea Sabasaba waone mambo mazuri,” alisema.

Dk Kijaji alisema zaidi ya kampuni 3,000 za Tanzania na 2,666 za nje ya nchi zimeshiriki maonyesho hayo hali inayosababisha kukuza ushirikiano wa kibiashara miongoni mwa nchi zilizoshiriki.

Aidha Dk Kijaji alisema kuwa kukutana kwa kampuni hizo na kushiriki kwa wingi zitasaidia kampuni za Tanzania kupata uzoefu kutoka katika kampuni hizo jambo litakalosaidia kuendeleza kampuni zao kisasa na kuongeza uzalishaji.

Alisema licha ya kampuni za ndani kupata ujuzi pia maonesho hayo yanafungua fursa kwa wawekezaji kuja nchini kuwekeza katika sekta mbalimbali.

“Naamini Maonesho haya ya 47 yataleta tija kwa kuwakaribisha wawekezaji wengine kuja nchini kuwekeza,”alisema Dk. Kijaji.

Alisema kampuni zàidi ya 150 kutoka nchini China kwa kutumia usafiri wa Shirika la Ndege la Tanzania kwaajili ya kuja kutembelea maonyesho haya.

“Hilo ndilo Rais wetu Samia Suluhu Hassan alisema anataka kufungua nchi na kuufungamanisha uchumini na shughuli zetu tunazofanya na ndio hili linaloendelea kutokea,” aliongeza Dk Kijaji.

Dk Kijaji alisema kutakuwa na makongamano mengi ya biashara ambayo yatatoa elimu na fursa za kibiashara wakati wa maonyesho na baada ya maonyesho ambapo kutakuwa na siku ya Irani, China na India kwa biashara ambapo siku hizo zitatangazwa fursa zinazopatikana kwenye nchi hizo, huku viongozi wakuu wa nchi hizo wakishiriki kwenye makongamano hayo.

Aidha, Waziri Kijaji aliwataka wafanyabiashara wa kitanzania kuendelee kuboresha na kubuni bidhaa nzuri kwa sababu wateja wapo na wanazipenda.

Naye Katibu Mkuu wa Chama Cha RPF Inkotanyi wa nchini Rwanda Komredi Wellars Gasamagera, alisema katika maonesho hayo kuna wafanyabiashara kutoka nchini Rwanda ambao wamefika kuonesha ubunifu wao mbalimbali.

“Tunashirikiana na nchi ya Tanzania katika mambo mengi ikiwemo namna ya kubadilishana ujuzi wa Biashara ili kukuza umoja na ushirikiano wa nchi zetu,” alisema Gasamagera.



No comments:

Post a Comment

Pages