HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 15, 2025

Anachoenda kuwaonyesha Dkt. Mwinyi Pemba

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Miradi mingi inatekelezwa Pemba kwa ajili ya wananchi na kati ya hiyo ipo ambayo ni ya kimkakati ambayo ni maji, miundombinu ya barabara na umeme kuelekea eneo la uwekezaji la Micheweni,

Ujenzi unaoendelea wa Bandari ya Mkoani ambako sasa makontena ambayo awali yalishukia Unguja, sasa yanapokelewa.

Banda la kupumzikia abiria, ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Pemba, ujenzi wa bandari ya Fumba Mjini itakayopokea meli za mizigo na boti za abiria  na ikumbukwe, Fumba Mjini ni kilometa chache baharini, kufika Mji wa Mombasa nchini Kenya.
Kulingana na Mhandisi Mshauri wa mradi, Abdallah Anova, TSh. Bilioni 7.7 zinajenga gati kwa ajili ya maegesho ya boti za abiria, uzio wa bandari, banda la kupumzikia abiria na huduma zingine.

Pia limetengwa eneo kubwa kwa ajili ya kuhifadhi makontena na bandari hiyo na kutoka bandarini hapo, kuna barabara za lami zinazokuongoza kuelekea Eneo Huru la Uwekezaji la Maziwang’ombe, Micheweni, mkoa huo wa Kaskazini Pemba.

Eneo hilo la kimkakati kumejengwa Kilometa 13 .5 za barabara za lami, kulizunguka  na kufika eneo hilo kutoka uwanja wa ndege Pemba si zaidi ya kilometa 45 na kikubwa zaidi umbali wote huo unatembea katika barabara za lam.

Kulingana na Meneja Uwezeshaji wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), Hamadi Othman Hamisi, katika eneo hilo, Block ‘A’ kumetengwa hekta 261/4 kwa ajili ya uwekezaji mchanganyiko.

Uwekezaji huo pamoja na mambo mengine, unaohusisha uhifadhi wa mazingira ni pamoja na kilimo viwanda, nyumba za kuishi, vyuo, ofisi na huduma zingine na tayari kuna wawekezaji kadhaa ambao wanasubiri vyeti kutoka mamlaka husika waanze utekelezaji wa miradi kusudiwa.

Eneo la Block ‘B’, kuna kuna hekta 540 zimetengwa kwa ajili ya uwekezaji mwingine na kwa ujumla kuna hekta 800 zinazosubiri uwekezaji na kuanzia zinatarajiwa kuzalisha  ajira zaidi ya 50 kwa wenyeji wakati wa kuanza ujenzi wa miradi husika.

Anasema meneja huyo, ajira hizo zitaongezeka zaidi kadiri shughuli za ujenzi zikapoendelea na zitakuwa maradufu mara baada ya miradi kukamilika na kuanza uzalishaji ambao Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM, Dkt, Hussein Mwinyi anataka uwe endelevu.

Kiwanda kuchakata mwani ambacho kimeanza kazi, barabara za kuingia mashambani, unenzi wa shule za ghorofa zenya vyumba vya kutosha klwa ajili ya wanafunzi, maabara za masomo yote ya sayansi na vifaa vyake na maktaba zinazosimamiwa na Maktaba Kuu ya Taifa.

Shule za majaribio ya matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) ambazo zina ubao janja (smart board) wa kufundishia ambao unamfanya mwalimu asiingie darasani na vitabu wala chaki katika kufundishia.

Mradi mkubwa wa maji na nishati ambao umelenga kuwafikia asilimia 90 ya wananchi wa Pemba katika mwaka huu wa fedha 2025/2026, umevutia wahisani wa Jumuia ya Ulaya (EU) na KFW kumwaga jumla ya Euro Milioni 75.9, serikali ikiwekeza Euro Milioni 25.

Maboresho makubwa yaliyofanyika Viwanja vya Michezo Gombani ambao sasa una viwanja vya nje vya mazoezi, upo tayari kwa ajili ya michuano yoyote ya Kimataifa na ni fursa nzuri pia kwa timu kuweka kambi au kuhamishia mechi zao hapo ni eneo jingine linalofungua ajira kwa vijana kupitia michezo.

Hospitali kubwa za kisasa zenye vipimo karibu vyote vya magonjwa mbalimbali katika wilaya zote, zikiwemo nyumba za wauguzi na madaktari katika Hospitali ya Abdullah Mzee, Mkoa Pemba ni sehemu ndogo sana ya miradi mikubwa iliyotekelezwa na Rais Dkt. Mwinyi, Pemba.

Mgombea huyo wa Urais (CCM), ambaye leo 15 Septemba 2025, anaenda kuomba ridhaa ya kuiongoza tena Zanzibar kufuatia uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu 2025, hiyo ni sehemu ya utekelezaji wake wa Ilani ya CCM na ahadi zake ambazo amezitimiza kwa zaidi ya asilimia 100.






 

No comments:

Post a Comment

Pages