DAR ES SALAAM, TANZANIA
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limeirudisha mechi ya ‘Kariakoo Derby’, kati ya Simba na Yanga mikononi mwa wamuzi wazawa, siku 83 tu tangu pambano baina ya miamba hiyo ilipochezeshwa na waamuzi wa kigeni kutoka nchini Misri, Juni 25, 2025 katika kuhitimisha Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/25.
Kesho Jumanne Septemba 16, Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania na Kombe la Shirikisho Tanzania, watakuwa wenyeji wa Simba katika mnyukano wa Ngao ya Jamii kuashiria ufunguzi wa msimu mpya wa mashindano ya ndani, pambano litalopigwa dimbani Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.
Kuelekea mechi hiyo itakayoanza saa 11 jioni, leo TFF imemtangaza Ahmed Arajiga kuwa mwamuzi wa mechi hiyo, ambayo Juni 25 ilichezeshwa na Mwamuzi Amin Mohamed Omar akisaidiwa na Moahmoud Abo El Regal na Samir Mohammed, kutoka Misri, alikotokea pia Ahmed Mahrous, ambaye alikuwa ‘fourth Official’ wa mechi hiyo.
Katika taarifa yake mchana wa leo, TFF imemtangaza Arajiga kuwa ‘pilato’ wa pmbano hilo, akisaidiwa na Watanzania wenzake Mohammed Mkono na Kassim Mpanga (wasaidizi namba moja na mbili, huku Ramadhani Kayoko akipangwa kuwa Mwamuzi wa Akiba. Soud Abdi yeye atakuwa Mtathmini Waamuzi.
Yanga wanashuka dimbani wakipania kuendeleza ubabe wao kwa Simba – ambao tayari wamewafunga katika mechi tano zilizopita, huku Wekundu wa Msimbazi wakiwa tayari kumalizauteja wao kwa Wana Jangwani kwa kuwaduwaza, wakichagizwa na maingizo mapya ya nyota wao waliotambulishwa Simba Day Septemba 10.
September 15, 2025
Home
Unlabelled
TFF yairejesha Kariakoo Derby kwa Waamuzi Wazawa, Arajiga Pilato kesho
TFF yairejesha Kariakoo Derby kwa Waamuzi Wazawa, Arajiga Pilato kesho
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.




No comments:
Post a Comment