Na Mwandishi Wetu, Katavi
MGOMBEA Mwenza wa Urais wa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, ameendelea kunadi Ilani ya Chama hicho ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030,ambayo kimsingi imelenga kwenda kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa maendeleo katika miaka mitano ijayo.
Dk.Nchimbi leo Septemba 9,2025 amewasili mkoani Katavi na kuhutubia wananchi katika Uwanja wa Maridadi,Mpanda mjini, kwenye mkutano wake wa hadhara wa Kampeni akitokea mkoani Rukwa.
Baada ya kuwahutubia Wananchi wa Mpanda Mjini,Balozi Nchimbi amewanadi Wagombea Ubunge wa majimbo mbalimbali ya Mkoa huo,akiwemo Mbunge wa jimbo la Mpanda mjini, Haidary Hemed Sumry pamoja na Madiwani.
Awali, Dkt. Nchimbi amewahutubia wananchi wa Majimoto,katika jimbo la Kavuu mkoani Katavi na kumnadi Mgombea Ubunge wa jimbo hilo Laurent Deogratius Luswetula pamoja na Madiwani.
Akiwa katika mkutano huo Dk.Nchimbi ametumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa CCM Dk.Samia Suluhu Hassan, Wabunge na Madiwani wa Chama hicho kwa kura za kishindo ifikapo Oktoba 29,2025.
September 09, 2025
Home
Unlabelled
DK. NCHIMBI AENDELEA KUINADI ILANI UCHAGUZI MKUU, KUOMBA KURA ZA KISHINDO KWA CCM
DK. NCHIMBI AENDELEA KUINADI ILANI UCHAGUZI MKUU, KUOMBA KURA ZA KISHINDO KWA CCM
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.



No comments:
Post a Comment