HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 10, 2025

Father' awa Rais wa Kwanza Azam FC, Popat Makamu wa Rais

BODI ya Azam FC imetangaza mabadiliko kimuundo na mfumo wa nafasi za juu za uongozi wa klabu hiyo, ambako nafasi ya Mwenyekiti imebadilika kuwa Rais, huku Nassor Idrisa 'Father,' akitangazwa kuwa Rais wa Kwanza Azam Complex, huku Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), Abdulkarim Amin 'Popat' akiteuliwa kuwa Makamu wa Rais. 

‎Mabadililo hayo yametangazwa rasmi jana usiku, ikielezwa kuwa Rais Nassor Idrisa atakuwa na Makamu wa Rais wawili, ambao ni Popat atashughulikia majukumu ya kikosi cha timu kubwa (Vice President - Senior Team), huku Omar Kuwe akiteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Akademi (Vice President - Academy).

‎"Kutokana na mabadiliko hayo, Afisa Mtendaji Mkuu mpya atatangazwa baadaye, kwa sasa Popat atakaimu nafasi hiyo. Aidha, Mkurugenzi wa Fedha, Abdulkarim Shermohamed 'Karim Mapesa,' ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Bodi," imesema taarifa hiyo iliyosisitiza kuwa mabadiliko hayo yameanza mara moja.

No comments:

Post a Comment

Pages