HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 09, 2025

Lawrence Mlaki Aahidi Kutatua Kero za Wananchi wa Kata ya Goba

Dar es Salaam – Uzinduzi wa kampeni za udiwani Kata ya Goba, Jimbo la Kibamba, umeendelea kushika kasi, huku Mgombea Ubunge wa Jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Angela Kairuki, akimnadi Diwani wa kata hiyo, Lawrence Mlaki.

Kairuki alisema wananchi wa Goba wana bahati ya kuwa na kiongozi anayesikiliza kero zao na kushirikiana nao. “Lawrence Mlaki ni kiongozi mchapakazi, anayesikiliza wananchi na kushughulika nao kwa karibu.

 Tunaomba kura nyingi, kwa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Mbunge na Diwani, ili tushirikiane kuleta maendeleo makubwa zaidi, ikiwemo kuhakikisha shule zinajengwa karibu na wananchi,” alisema Kairuki huku akishangiliwa na wafuasi wa CCM.

Diwani Mlaki alitumia jukwaa hilo kueleza changamoto zinazowakabili wakazi wa Goba na mikakati yake ya kuzitatua. Alisema kero kubwa ni upatikanaji wa maji safi katika mitaa ya Matosa, Kuguru, Kulalangwa na Kibululu. Aidha, aliahidi kushughulikia suala la daladala, masoko ambapo eneo jipya tayari limepatikana.

Mlaki alisema: “Michezo ni kichocheo cha afya tutashulikia upatikanaji wa viwanja pia  urasimishaji wa ardhi, kujenga zahanati na kuongeza vituo vya ulinzi ili wananchi wa Goba waishi kwa amani na usalama.”

Aidha Diwani huyo pia aliahidi kushughulikia mikopo kwa wazee, kuboresha vivuko,  alisisitiza utawala bora na kupiga vita rushwa, na aliahidi kuweka vikao vya mara kwa mara na mabalozi pamoja na wananchi ili kuhakikisha ushirikishwaji wa kila mmoja.

Akihitimisha hotuba yake, Mlaki aliwaomba wananchi wa Goba: “Jitokezeni kwa wingi siku ya kupiga kura, ili tuihakikishe CCM inapata ushindi wa kishindo. Tumchangue Rais Samia Suluhu Hassan, Mbunge na Udiwani.




No comments:

Post a Comment

Pages