HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 14, 2025

Dkt. Mwinyi azindua kampeni, ataja vipaumbele vyake

 Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Mgombea wa Urais Zanzibar kwa tiketi ya CCM,  Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameahidi kuendeleza zaidi yale aliyoyaanza ikiwa ni pamoja na kuvuka lengo la Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025-2030 la ajira 350000 kwa viiana.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho viwanja vya Mnazi Mmoja, Unguja 13 Septemba 2025 Dkt. Mwinyi alisema kuwa atafanya hivyo kwa kuwa mwelekeo kiuchumi Zanzibar upo vizuri.

Alisema uwekezaji unaofanywa hivyo sasa ikiwa ni pamoja na viwanda vinavyojengwa vitainua uchumi na kuzalisha ajira nyingi zaidi hususan kwa vijana.

"Uchumi wa Zanzibar umekua kwa asilimia 7.4, tunaenda vizuri" alisema na kuongeza kuwa miaka mitano ijayo utaimarika zaidi.

Alisema ataongeza mafungu ya pesa kwenye mikopo isiyo na riba inayotolewa na serikali.

Pia hifadhi ya chakula, mafuta na gesi ni vipaumbele vyake na maendeleo anayofanya si ya kibaguzi, hayachagui Pemba wala Unguja.

Awali akizungumza katika uzinduzi huo, Rais Mstaafu Mohamed Shein alisema kuwa kukopa kwa ajili ya maendeleo ndio ustaarabu wa kisasa wa dunia na hata mataifa makubwa yanakopa.

Dkt. Shein alitaka maendeleo yanayoletwa na Dkt. Hussein Ali Mwinyi yanatakiwa kuungwa mkono na si ya kubeza.


 

No comments:

Post a Comment

Pages