NA DENIS MLOWE, IRINGA
MBUNGE
Mteule wa Viti Maalum Vijana Taifa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)
kutoka mkoa wa Iringa, Jasmine Ng’umbi, ameahidi kutumia nafasi yake
bungeni kuhamasisha na kusukuma mbele miradi inayowagusa moja kwa moja
vijana na wanawake, ili kuongeza fursa za maendeleo kwa makundi hayo.
Akizungumza
leo wakati Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira,
akizindua kampeni za wagombea ubunge na udiwani katika majimbo ya
Kalenga na Iringa Mjini, Jasmine alisema anaingia bungeni akiwa na azma
ya kuhakikisha vijana na wanawake wanapata nafasi kubwa zaidi kiuchumi
na kijamii.
Jasmine pia aliwataka wananchi wa
Iringa na Watanzania kwa ujumla kuhakikisha wanampa kura za kishindo Dk
Samia, wabunge na madiwani, akisema chama hicho kimeonesha kwa vitendo
kwamba kina uwezo wa kusukuma maendeleo kwa wote bila ubaguzi.
“Rais
Samia ameonesha mfano wa uongozi wa vitendo. Sasa ni jukumu letu
kuendeleza kasi hiyo kwa kuhakikisha CCM inaendelea kupewa ridhaa ya
kuongoza, ili vijana, wanawake na Taifa kwa ujumla waendelee kufaidika,”
alisisitiza.



No comments:
Post a Comment