HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 15, 2025

Dkt. Mwinyi: Sijasikia wanataja shule wala barabara

Na Mwandishi Wetu, Pemba


Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi anasema amesikiliza 'Crip' ya uzinduzi mkutano wa ACT Wazalendo mwanzo hadi mwisho lakin, hajasikia lolote kuhusu elimu wala barabara zaidi ya lawama, fitina, chuki, ubaguzi na uzushi.

Akizungumza wakati wa mkutano wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi CCM, Pemba, Dkt. Mwinyi alisema hajasikia wakitaja watafanya nini kwenye elimu wala barabara jambo linaloonyesha kuwa hawana sera hivyo wananchi wawakatae.

"Wakataeni hao wanaohubiri mifarakano badala ya amani, umoja na mshikamano" alisema na kutaja mafanikio 11 yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitano ya amani na utulivu kwa waZanzibari.

Alisema bila amani na utulivu uliokuwepo ni vigumu kupata maendeleo kama hayo yaliyofikiwa.

Alisema pamoja na kuendeleza kile  ambacho amekianza akipata ridhaa ya wananchi watarajie makubwa zaidi.

Alisema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar sasa kutoa hatimiliki za mashamba ya karafuu ili waweze kuyasafisha na serikali itanunua karafuu na vitaanzishwa viwanda vya kuichakata ili kuiongezea thamani hivyo kufanya wakulima kulipwa vizuri zaidi.

Alisema hatimiliki itasaaidia wamiliki ikitokea wakafariki wanaobaki waweze kurithi na kuendelea kunufaika nayo.

"Kuhusu utalii Pemba tunataka uwekezaji mkubwa, zijengwe hoteli kubwa zenye hadhi ya juu na hatutaki utalii wa vishuka" alisema.

Alibaimisha kuwa 25 Septemba 2025, anaikabidhi barabara ya Chake/Mkoani kwa mkandarasi sanjari na ujenzi wa Uwanja wa ndege wa Pemba ambao unaenda kuwa wa kimataifa hivyo kufanya kuwe na ndege za moja kwa moja toka Ulaya na kwingineko.

"Ukikamilika kutakuwa na ndege za moja kwa moja toka Ulaya kuja Pemba" alisema.

Alibainisha kuwa bei za vyakula zimeimarika baada ya bandari ya mkoani kuanza kupokea meli zenye makontena badala ya awali mizigo kushushwa Unguja, Dar es Salaam au Mombasa kisha kuletwa Pemba hivyo kufanya bei kuwa juu sababu ya uchukuzi. 



No comments:

Post a Comment

Pages