MUARGENTINA Miguel Gamondi, ameipa Singida Black Stars taji la kwanza katika historia yao, baada ya kuiongoza timu hiyo kutwaa taji la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Kagame Cup 2025), wakiichapa Al Hilal Omdurman ya Sudan kwa mabao 2-1 katika fainali.
Ukiondoa Gamondi, shujaa wa Singida Black Stars leo ni Nyota wa kimataifa wa Zambia, Clatous Chota Chama 'Mwamba wa Lusaka,' aliyefunga mabao yote mawili - moja katika kila kipindi na kufungua msimu kwa neema ya taji, siku tano tu kabla ya kupeperusha bendera ya Tanzania katika Kombe la Shirikisho Afrika (CAF CC 2025/26).
Chama, ambaye msimu uliopita alichezea Young Africans 'Yanga,' aliitangliza Singida Black Stars mapema dakika ya 20, kabla ya Taha Abdelrazig kuisawazishia Al Hilal dakika 11 baadaye na timu zote kwenda mapumziko kwa sare ya bao 1-1.
Akiwa katika kiwango cha juu leo, Chama maarufu pia kama Triple C, aliifungia Singida Black Stars bao la pili kunako dakika ya 57 ya mtifuano huo kwenye dimba la Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni 'KMC Complex' hivyo kuiingiza timu yake kwenye rekodi ya kuwa moja ya klabu zilizowahi kutwaa ubingwa wa michuano hiyo inayodhaminiwa na Rais wa Rwanda, Paul Kagame.
Baada ya ushindi huo, Singida Black Stars inaondoka moja kwa moja nchini, kwenda Kigali, Rwanda ambako jioni ya Jumamosi ya Septemba 20 watakuwa wageni wa Rayon Sports ya huko, katika mechi za raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF CC 2025/26).
September 15, 2025
Home
Unlabelled
Singida Black Stars bingwa Kombe la CECAFA, Chama shujaa
Singida Black Stars bingwa Kombe la CECAFA, Chama shujaa
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.



No comments:
Post a Comment