HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 10, 2025

DKT.NCHIMBI ASIMAMA KUWASALIMIA WANANCHI WA NSIMBO AKIELEKEA WILAYA YA MLELE -KATAVI

MGOMBEA Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John  Nchimbi, akiwasalimia Wanachi wa kata ya Katumba,Halmashauri ya ya Nsimbo leo Jumatano Septemba 10,2025, wakati akielekea  Wilaya ya Mlele katika Jimbo la Kavuu, kuhutubia Wananchi kwenye mkutano wake mkubwa wa hadhara wa Kampeni mkoani Katavi.

Baada ya kuwasalimia Wananchi wa Nsimbo, Dkt. Nchimbi aliwanadi Wagombea Ubunge wa majimbo mbalimbali ya  Mkoa huo,akiwemo mgombea Ubunge wa jimbo la Nsimbo,Anna Richard Lupembe  pamoja na Madiwani.

Dkt. Nchimbi ameendelea kunadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030,ambayo kimsingi imelenga kwenda kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa Maendeleo katika miaka mitano ijayo.

Aidha amekuwa akitumia  nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa CCM,Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan, Wabunge na Madiwani wa Chama hicho kwa kura za kishindo ifikapo Oktoba 29,2025.


 

No comments:

Post a Comment

Pages