JARIBIO la Kikosi cha timu ya soka ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', kukusanya alama sita katika mechi mbili za mwisho za Kundi E kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026, limegonga mwamba, baada ya jioni hii kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Niger, kwenye dimba la Amaan Complex Zanzibar.

Bao pekee katika mechi limewekwa kimiani dakika ya 58 na Daniel Sosah, nyota wa kimataifa wa Niger, mzaliwa wa Ghana, anayekipiga klabu ya Aktobe FC ya Kazakhstan, hivyo sio tu kuipoka pointi tatu Taifa Stars, bali kulipa kisasi cha kufungwa 1-0 kwa bao la Charles M'mombwa mjini Marrakech, Morocco, Novemba 18 mwaka jana.
Taifa Stars inayonolewa na Hemed Suleiman 'Morocco', ilishuka dimbani visiwani Zanzibar ikiwa na kumbukumbu ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Congo-Brazzaille katika mechi iliyopita, hivyo kujipoteza rasmi katika Barabara ya kuelekea fainali zinazoandaliwa kwa ushirikiano wa nchi za Canada, Marekani na Mexico.
Baada ya kukosa nafasi ya kufuzu moja kwa moja katika fainali hizo, tumaini la Taifa Stars lilikuwa ni kushinda mechi mbili zilizobaki ikiwemo hiyo ya Niger na Zambia mwezi ujao, lakini kipigo hicho kimeondoa uwezekano wa kumaliza na pointi zitakazokuwa na manufaa kuelekea kuingia 'top four' ya Washindwa Bora 'best loosers.'
September 09, 2025
Home
Unlabelled
Niger yaitambia Taifa Stars New Amaan Zanzibar, yalipa kisasi
Niger yaitambia Taifa Stars New Amaan Zanzibar, yalipa kisasi
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.



No comments:
Post a Comment