HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 09, 2025

SMZ kuondoa tatizo la maji Pemba

 Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

ZAIDI ya asilimia 80 ya wakazi wa Pemba na vitongoji vyake, wanatarajia kupata huduma ya maji kufuatia uwekezaji mkubwa unaotekelezwa visiwani humo na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Benki ya Exim na wadau maendeleo ikiwemo Jumuia ya Ulaya (EU) na Benki ya Dunia (WB).

Akizungumza na habari Mseto kwa njia ya simu, Ofisa Mdhamini wa Wizara ya Maji, Nishati na Madini Zanzibar, Suleiman Hamad Omary alisema serikali imelenga kutatua changamoto hiyo kwa wakazi wa visiwa hivyo na kiasi cha TSh. Bilioni 68 zimetengwa katika Bajeti ya Serikali 2025.

Alisema Mdhamini Omary kuwa Jumuia ya Ulaya (EU), imetoa mkopo wenye thamani ya Euro Milioni 616 wakati Benki ya Exim ambayo awamu ya kwanza wametekeleza miradi ya maji Unguja. Itatumia  Dola za Kimarekani Milioni 17.5 kusambaza maji na kujenga matenki ya kuhifadhia.

Benki ya Dunia itatekeleza mradi wenye thamani ya Dola za Marekani zaidi ya Milioni 15 na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imechangia Tsh.Milioni 35 katika uteekelezaji wa miradi hiyo ambayo kulingana na Malengo ya serikali kumaliza kabisa changamoto ya upatikanaji  maji Pemba kwa asilimia 100 ndani ya miaka mitatu ijayo.

Katika ziara ya hivi karibuni ya wanahabari katika Tenki kubwa la Maji, eneo la Kiwani Kendwa mdhamini huyo alieleza kuwa serikali katika mwaka wa fedha 2025, imetenga Tsh.Bilioni 68 kwa ajili ya miradi ya maji Unguja na Pemba na hatua hiyo inaenda kuyapatia maji ya uhakika maeneo ambayo yalikuwa yanapata kwa mgawo.

Ofisa mdhamini Omary alibainisha kuwa mathalani tenki hilo la Kiwani Kendwa lenye ujazo wa lita milioni 1 linahudumia Sheia kubwa mbili ambazo ni Kiwani Vijijini na Kiwani Sokoni ambako kuna vitongoji vya Mchakweni, Bomani na Tasini na ambavyo awali havikuwa vinapata kabisa kutokana na ongezeko la watumiaji wa huduma.

 “Pia kuna wawekezaji kutokana China ambao tayari wameanza wapo katika hatua za awali ambao wao wanashughulika na eneo la Mtambwe yote, Kusini na Kaskazini ambako pia wanapeleka umeme” alisema na kuwataka watendaji kuendana na kasi ya Rais Dkt. Hussein Mwinyi katika utekelezaji wa miradi  ya maendeleo ya wananchi.



 

No comments:

Post a Comment

Pages