HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 11, 2025

Rais Samia apiga simu Simba Day, mashabiki walipuka

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amepiga moja kwa moja 'live,' wakati wa Tamasha la Kilele cha Siku ya Simba 'Simba Day 2025.' 

‎Rais ameupongeza uongozi wa klabu ya Simba na mashabiki wao kwa tukio hilo kubwa lililojaza dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam,huku akiwataka kudumisha mshikamano bainanya watendaji wa timu na wafuasi wao.

‎Rais Samia alipiga simu hiyo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, aliyekuwa akizungumza na maelfu ya wahudhuriaji hao, baada ya kumaliza kuzungumza Waziri wa Maji, Jumaa Awesu, ambaye ni Mgeni Rasmi wa Simba Day 2025.

‎"Nafuatilia tamasha lenu kwenye runinga, namuona Mwenyekiti hapo na wengine wote. Niwapongeze mashabiki wa Simba kwa mwitikio mkubwa na nitumie nafasi hii kuwatakia kila la kheir," alisema Rais Samia kupitia simu ya Msigwa, iliyounganishwa na kipaza sauti na kuibua shangwe zito la mashabiki, hasa waliovaa kanga na 't-shirt' za Rais Samia. 




No comments:

Post a Comment

Pages