Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Regina Chonjo, akifunga kikao cha wadau walioshiriki kuandaa taarifa ya Nchi ya Utekelezaji wa Mkataba wa Kimataifa wa kutokomeza vitendo vya ubaguzi dhidi ya wanawake uliofanyika mjini Morogoro.
Na Mwandishi Wetu, Morogoro
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Bi. Regina Chonjo
amewataka wadau wa haki na utetezi wa wanawake kuendeleza juhudi za Serikali
ili kuhakikisha wanawake wanalindwa dhidi ya ubaguzi wa aina yoyote na
kushiriki katika fursa za maendeleo na ustawi wao.
Bi. Chonjo alisema hayo wakati wa
kuahirisha Kikao cha wadau wa Kitaifa waliokutana mjini Morogoro kwa lengo la
kuboresha Taarifa ya Nchi ya Utekelezaji wa Mkataba wa Kimataifa wa Kutokomeza
aina zote za ubaguzi Dhidi ya Wanawake (CEDAW).
Aidha Bi. Chonjo aliwapongeza wadau
kwa kuweza kuainisha mafanikio yaliyofikiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania katika kuzuia ubaguzi dhidi ya wanawake na wasichana kwa kipindi
cha mwaka 2015 hadi 2019 akilitaja jambo hilo kuwa limetokana na utendaji wa
pamoja.
’’Kazi hii ya kuandaa Taarifa ya Nchi
ambayo mumeifanya kwa muda wa siku tatu itaboresha shughuli zilizofanyika na
kuonesha jinsi Tanzania ilivyotekeleza masuala ya kutokomeza ubaguzi dhidi ya
wanawake na pia kuwawezesha kiuchumi, kisiasa na kijamii’’. Aliongeza Bi.
Chonjo.
Aidha Bi. Chonjo pia alisema idadi ya wanawake nchini
Tanzania ni kubwa ukilinganisha na idadi ya wanaume uku akitaja takwimu
zinaonesha kuwa kuna takriban asilimia 51 ya wanawake ukilinganisha na wanaume
na kati ya hao 80% wanaishi vijijini wakijiajiri katika shughuli za kilimo,
hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kuwalinda wanawake dhidi ya ubaguzi na aina zote
za ukatili wa kijinsia ili kushiriki nafasi za maendeleo.
’’Tukitambua kuwa idadi ya Wanawake nchini ni
kubwa kwa asilimia 51 ukilinganisha na idadi ya wanaume hoja hii inakuwa msingi
wa kuwekeza katika kukuza ushiriki wa wanawake ambapo takriban asilimia 80 ya
wanawake hao wanaishi vijijini wakiwa wamejiajiri katika sekta ya kilimo, hivyo
kuna uhitaji mkubwa wa kupinga ubaguzi dhidi ya wanawake’’.Alisisitiza kiongozi
huyo wa Wilaya.
Aidha Bi. Chonjo alizitaja juhudi za
serikali katika kupambana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake nni
pamoja na kuanzisha Madawati ya Jinsia na Watoto 420 katika Vituo vya Polisi kwa lengo la kuwezesha kupata haki na huduma stahiki kwa wanawake na kuongeza kuwa madawati haya yameongeza ari ya wananchi kujiamini na kuvunja ukimya katika utoaji taarifa za vitendo vya ukatili kwenye maeneo ya jamii.
Aidha Bi. Chonjo alivitaja Vituo vya pamoja vya kutoa huduma kwa wahanga wa
ukatili wa kijinsia kuwa vimeanzishwa katika mikoa sita ya Tanzania Bara
ambavyo ni Dar es
Salaam, Pwani, Mwanza, Mbeya, Iringa na Shinyanga vimewesha utoaji wa huduma stahiki kwa waathirika akivitaja kuwa hatua muhimu
iliyochokuliwa na serikali kupambana na vitendo vya ukatili hapa Nchini.
Bi. Chonjo alitaja hatua nyingine
iliyochukuliwa na Searikali kupuna na vitendo vya ukatili kuwa ni kufanya marekebisho ya Sheria ya Elimu na
kulifanya kosa la kumpa mimba au kuoa au kuolewa mwanafunzi wa shule za msingi
na sekondari kuwa kosa la jinai na pale inapothibitika adhabu yake ni kifungo
cha miaka 30 marekebisho haya yamesaidia kupunguza
matukio ya mimba za utotoni.
Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya
Maendeleo ya Jinsia Bibi Mboni Mgaza ameeleza kuwa Taarifa hii ya Tisa ya
Utekelezaji wa Mkataba wa Kimataifa wa Kutokomeza aina zote za ubaguzi Dhidi ya
Wanawake (CEDAW)itawasilishwa Umoja wa Mataifa Mwezi Machi 2020 ikiwa
imeunganisha taarifa ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar
No comments:
Post a Comment