HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 06, 2022

Timu za Taifa za Pool zatinga nusu fainali Wanaume na Wanawake

TIMU za Taifa za mchezo wa Pooltable Waanaume na Wanawake wamefanikiwa kuingia nusu fainali baada kuvuka hatua na makundi kwa timu za Wanaume na Wanawake.

Timu ya Wanaume imefanikiwa kuingia nusu fainali kwa kuzifunga timu ya Kenya 13-9, Uganda 13-8 na Zimbabwe 13 -6.

Nusu fainali ambayo kwa sasa inaendelea ni Tanzania na Afrika Kusini wakati nusu fainali ya pili ni wenyeji Zambia na Uganda.

Upande wa Wanawake pia Tanzania imefanikiwa kuingia nusu fainali ambapo inacheza na  Afrika Kusini pia.

Kocha wa timu ya Taifa ya Pool, Denis Rungu mwenye uraia wa Zambia ametamba kurudi na ushindi wa kishindo Tanzania kwa jinsi alivyoandaa vikosi viwili vyote vya timu ya Wanaume na Wanawake.

Nchi saba zimefanikiwa kushiriki mashindano hayo ya Pool Afrika ambazo ni Afrika Kusini, Zimbabwe, Kenya, Uganda, Swaziland, Tanzania na Wenyeji Zambia ambapo Nchi zote zimewakilisha na timu ya Wanaume na Wanawake.

Mahindano hayo yanatarajiwa kumalizika kesho huko Lusaka Zambia.

 

 

 

 

No comments:

Post a Comment

Pages